NYG GROUP SONGEA ni Shirika la Kijamii lililosajiliwa (CBO Na. NA-6913) lenye makao yake Songea, Tanzania.
Shirika linaendesha shughuli za huduma, muziki na maendeleo ya jamii, ikiwemo NYG WORSHIP na NYG MUSIC HUB.
NYG GROUP SONGEA pia imesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na imepewa kibali cha kuendesha shughuli za sanaa chini ya Namba ya Usajili BST-9684-2026-1645. Kibali cha BASATA ni halali kuanzia 10 Septemba 2026 hadi 10 Septemba 2027.
NYG GROUP SONGEA ilianzishwa na inaongozwa na Eliud Davies Bilal.
Kujenga jamii iliyobadilishwa, iliyohamasishwa na kuwezeshwa kupitia imani, muziki, ubunifu na maendeleo ya jamii.
Kutumia imani, muziki, vyombo vya habari na shughuli za kijamii kuhamasisha, kuwezesha na kuleta mabadiliko chanya katika maisha.
Likes + Views = Trending Points
NYG WORSHIP
Kikundi cha waimbaji wa Injili kutoka Songea, Tanzania.
Gusa kufungua Biography
NYG WORSHIP ni kikundi cha waimbaji wa Injili kutoka Ruvuma, Songea, Tanzania. Kilianza huduma ya uimbaji mwaka 2025.
Msukumo wa ndani katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji mbali na kufundisha neno na kulihubiri.
Msukumo wa kimuziki: Hillsong Worship.
Changamoto kubwa ilikuwa ni kwenye ku-shoot video ya wimbo wa SEMA NENO, ulikuwa na gharama kubwa na namna ya kuufanyia promotion kulikuwa na njia nyingi ngeni kwetu.
TEMBEA NA YESU β mwaka 2025.
Tuna nyimbo 6 ambazo ni EP yetu ya kwanza inayoitwa LIGHT OF THE WORLD.
Zote ni nzuri na zina ujumbe, ila kwa tofauti na kwa nyakati tofauti. Zinafaa watu wote wenye hali zote.
Jina NYG limekua na kuenea karibia kila mahali na tumefanikiwa kupeleka ujumbe wetu juu ya Kristo kwa TV, radio, social platform zote na kuwafikia watu wengi wakapokea neno la Kristo kupitia nyimbo zetu.
Tumefanikiwa kuwa na tovuti inayotangaza kazi zetu na kazi zingine za waimbaji kama sisi.
Tumeshirikiana na OBBY ALPHA katika wimbo wa SEMA NENO.
Sisi ni wajasiriamali, tunalima, tunafuga, tunafanya sanaa mbalimbali za ufundi n.k.
Neno la Kristo lina nguvu saba unapolipeleka kwa watu kwa njia ya uimbaji sababu kila mtu atavutiwa kusikiliza kuliko kuwasubiri watu waje makanisani.
LIGHT OF THE WORLD EP
Tunataka kuwafikia watu wengi zaidi na kwenda duniani kote na kuitangaza injili ya Bwana bila mipaka ya kidini, kikabila na kidhehebu.
Tunataka kuwa chanzo cha mafanikio makubwa kwa waimbaji ambao wapo ndani ya NYG WORSHIP na walio nje yetu.
Wasikate tamaa kutokana na changamoto zilizopo! Wasonge mbele wakitumia kidogo walichonacho kukua na kuongezeka! Inawezekana kwake aaminiye!
Nataka kuitangaza EP yetu mpya na kuifikisha kote duniani kupitia tovuti hii.
YouTube: NYG WORSHIP LABEL
Facebook: NYG WORSHIP Facebook
AZZO DREY
Msanii wa muziki wa Injili.
Gusa kufungua Biography
Andrea Arthur, anayefahamika kisanii kama AZZO DREY, ni msanii binafsi wa muziki wa Injili kutoka Songea, Ruvuma, Tanzania. Alianza huduma yake ya uimbaji mwaka 2019.
Upendo wake kwa Mungu ulimhamasisha kuhubiri Neno kupitia nyimbo za Injili. Apostle Eliud Bilali ni mfano wake wa kuigwa katika kumtumikia Mungu.
Wimbo wake wa kwanza ni HALLELUYA, uliotoka mwaka 2025. Hadi sasa ametoa nyimbo 10 na hana album wala EP.
Changamoto kubwa imekuwa kupata sapoti ya kutosha. Amefanikiwa kujulikana ndani na nje ya mkoa wake.
Ameshirikiana na NYG WORSHIP LABEL. Pia anajishughulisha na Music Production.
MAOMBI ni wimbo unaoelezea jinsi Mungu anavyotenda sawasawa na mapenzi yake.
Anatamani kuwahamasisha vijana kumuabudu Mungu katika roho na kweli, na kufikisha huduma yake Tanzania nzima na duniani kote.
Wakaze kumpenda Mungu, naye atawainua.
APOSTLE ELIUD BILALI
Mwimbaji wa Injili, Mchungaji na Balozi wa Amani Duniani.
Gusa kufungua Biography
Apostle Eliud Davies Bilal, anayefahamika kisanii kama Apostle Eliud Bilali, ni msanii binafsi wa muziki wa Injili. Kwa asili anatokea Lushoto, Tanga, Tanzania, na kwa sasa anaishi Songea, mkoani Ruvuma. Alianza rasmi huduma ya uimbaji mwaka 2010.
Upendo wa uimbaji ulitoka ndani ya moyo wake, bila kushinikizwa na mtu. Katika safari yake amepata msukumo kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Mungu, akiwemo Pastor Gwakisa Mwaipopo.
Mwaka 2010 alitoa nyimbo zake za mwanzo, YESU NI MALI YANGU na EVERYTHING, ambazo zilisikika mbali. Hadi sasa ana album tatu na single zaidi ya kumi zinazotolewa pia katika mfumo wa EP za mfululizo.
Changamoto kubwa aliyoipitia mwanzoni mwa huduma yake ilikuwa kukosa maarifa ya kutosha katika kipindi hicho.
I'M STILL GOING ON (BADO NINAENDELEA) ni wimbo anaoupenda kwa sababu una ujumbe wa kumtia moyo kuendelea kusonga mbele.
Kupitia uimbaji amefanikiwa kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa watu wengi, kufahamiana na watu mbalimbali na kupata furaha katika huduma yake.
Ameshirikiana na NYG WORSHIP pamoja na waimbaji wengine, wakiwemo Irene Mhando na Obby Alpha katika kazi za muziki wa Injili.
Mbali na uimbaji, ni Balozi wa Amani Duniani, Mchungaji na kiongozi wa NYG, pamoja na kuwa mtaalamu wa afya ya kinywa na meno.
"Mpendeni Yesu, inalipa."
Katika malengo yake ya miaka mitano ijayo, ametaja ndoto ya kuwa na ghorofa tanoπ . Anaendelea na safari ya huduma na maendeleo yake binafsi.
UNAWEZA - AI VERSION ni wimbo uliowasilishwa kwa ajili ya kutangazwa kupitia NYG CENTER - ARTIST OF THE WEEK.
Tazama NYG WORSHIP kwenye YouTube
"Wakaze na waombe Mungu, hakuna vya rahisi! Kujituma na kuthubutu ndo njia."
Facebook - Apostle Eliud Bilali
Audiomack - Apostle Eliud Bilali
Safari ya Apostle Eliud Bilali katika muziki wa Injili ni sehemu ya huduma yake ya kumtumikia Mungu na jamii. Kupitia nyimbo, uongozi wa kiroho na shughuli za kijamii, anaendelea kufikisha ujumbe wa imani, tumaini na upendo.
"Mpendeni Yesu, inalipa."
Karibu NYG FRIENDS! Pata fursa za kazi, jiunge na jumuiya yetu na ushiriki katika programu mbalimbali.
FUNGUA NYG MARKET PLACE →
Sikiliza matendo makuu ya Mungu katika maisha ya waamini.
Shuhuda zinapakiwa...
Jadili shuhuda kwa kutaja namba yake.
Mtumishi wa Mungu na Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Nuru Yangβaa Gizani β
NYG GRACELAND CENTER, Msamala, Songea, Tanzania,
Balozi Apostle Bilali, ametangaza rasmi
Oktoba 2026 kuwa Mwezi wa Kitume.
Kilele chake kitakuwa tarehe 25/10/2026, ambapo
Ibada Kuu ya APOSTOLIC DAY itafanyika.
Katika kikao chake na watenda kazi Jumamosi hii, Apostle Bilali
amethibitisha kuwa mwezi huu utakuwa na misheni mbalimbali, zikiwemo
kuwatembelea wafungwa na kuwapatia mahitaji muhimu,
kuhubiri Injili mitaani na kufanya semina.
Mwezi wa Kitume utahitimishwa kwa Ibada Kuu pamoja na
Tamasha la Sifa tarehe 25/10/2026.
Waimbaji kutoka NYG WORSHIP watashiriki na
kulipamba tamasha hilo.
Apostle Bilali ametoa mwongozo wa namna ya kuenenda katika Mwezi
huu wa Kitume na amewakaribisha watu wote kushiriki matukio
mbalimbali yatakayofanyika katika mwezi huu.
VITABU 5 VYA KUJENGA UCHUMI WAKO
0755 498 731.
Karibu utuletee wimbo wako mpya na bora ili
usikike, utambulike na kupata nafasi ya
ku-trend kwenye kurasa zetu!
Wasiliana nasi whatsup 0755498731 na ututumie link ya YouTube
ya wimbo wako kwa ajili ya ukaguzi.
Wimbo utakaokidhi vigezo vyetu
utaidhinishwa na kutangazwa.
Karibu kusikiliza Neno la Mungu na maombi kila Jumatatu mpaka Ijumaa, saa 7:00 mchana! Apostle Bilali anakuwa LIVE STREAM hapahapa!
NYG CENTER inaheshimu na kulinda faragha ya watumiaji wa tovuti yetu. Taarifa zozote zinazotolewa kupitia huduma za tovuti, ikiwemo NYG LIVE CHAT, zitatumika kwa madhumuni ya mawasiliano na kuboresha huduma zetu.
Watumiaji wanashauriwa kutotuma taarifa nyeti binafsi kupitia sehemu ya mazungumzo ya moja kwa moja.
Hatutauza au kutoa taarifa binafsi za watumiaji kwa watu wengine kwa madhumuni ya kibiashara bila ruhusa, isipokuwa pale inapohitajika kwa mujibu wa sheria.
Kwa maswali kuhusu faragha na matumizi ya tovuti, wasiliana nasi kupitia: info@nygmusichub.com